FLAVIANNA MATATA NA RANGI ZA KUCHA
Mwanamitindo flaviana matata anaeishi na kuendesha shughuli zake za mitindo huko nchini marekani ambae pia mmiliki wa shirika la kusaidia watoto wasiojiweza lijulikanalo Kama flaviana matata foundation(FMF),amekuja na ujio mpya wa bidhaa za rangi za kucha zinazoitwa LAVY.Mrembo huyo amezindua na kuzitambulisha bidhaa hizo leo hapa jijini dar es salaam.bidhaa hizo zimeanza kuuzwa rasmi leo na zinapatikana katika maduka ya shearillusionsafrica na Picasso beauty studio.mrembo huyo ameongeza kuwa anampango wa kutangaza bidhaa hizo kimataifa zaidi kwan zina ubora unaostahili na kuomba watanzania na watu wengine kumuunga mkono katika safari yake hiyo na kuwaahidi wategemee mambo mazuri zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment