AINA ZA NGONZI NA MATUNZO YAKE

Kuna aina nne za ngozi (muonekano) kwa jinsia zote mbili yani kike na kiume.Aina zote hizi zinaitaji matunzo tofauti tofauti kulingana na mtu mwenyewe, unaweza fanya mwenyewe au Kama una uwezo zaidi kwenda kufanyiwa sehemu maalum Kama saloon.Tukumbuke pia kwenye matumizi ya vitu Kama mafuta na losheni( lotion) za mwili ni muhimu kuzingatia una ngozi ya aina gani na hata bidhaa zenyewe huwa zimeelezwa matumizi sahihi yaani inastahili ngozi ya aina gani, kwa hilo ni muhimu zaidi kuzingatia ili kupata muonekano sahihi unaoitaji.Aina ya kwanza Kama inavyoonekana pichani ni ngozi kavu(Dry skin),yaani isiyo na mafuta, watu wenye aina hii ya ngozi hupata shida sana kwa sababu ngozi inapokua kavu husababisha kuvutana,mipasuko,ugumu na kusinyaa!watu wenye aina hii ya ngozi hushauliwa kupaka lotion au mafuta ya kulainisha ngozi(for dry skins) ili kuwafanya wawe na muonekano ng'aavu na wakuvutia. Aina ya pili ni ngozi ya kawaida(Normal skin),aina hii ya ngozi inakua na mafuta kidogo na ukavu kidogo ni wachache sana wenye aina hii wanaojigundua kua nyuso zao zinamuonekano mara mbili.mtu yeyote mwenye aina hii ya ngozi anashauliwa kupaka mafuta yakawaida yasiokua makavu sana na wala yenye mafuta sana Kama nilivyoeleza hapo mwanzo mafuta ama losheni( lotion) mara nyingi hua zimeandikwa kama itakuwia vigumu sana kusoma ni vizuri kumuuliza muuzaji wa bidhaa hiyo. Aina ya tatu ni ngozi ambayo katikati hua inamafuta yaani paji la uso kushuka mapaka kwenye pua na pembeni kuwa na ngozi ya kawaida(Combination skin),aina hii ya ngozi inaitaji umakini sana kwa sababu unaweza dhani ngozi yako ni ya mafuta kumbe sio yote ni vizuri na ni salama kuhusisha wataalam wa urembo kwenye uchaguzi wa mafuta au losheni(lotion) epuka sana kupaka vitu vyenye mafuta na vikavu pia,yaani iwe ya kawaida. Aina ya nne ni ngozi yenye mafuta(Oil skin),aina hii ya ngozi haiitaji kabisa kupakwa mafuta ama losheni zitakazo ongeza mafuta zaidi  kwenye ngozi kwa sababu itazidisha zaidi na ni vizuli kutumia losheni(lotion)kavu ili kupunguza mafuta hayo na kuipa ngozi muonekano sahihi.Hakikisha unatumia bidhaa sahihi kwa aina yako ya ngozi na epuka kutumia bidhaa zitakazo badili(chubua) ngozi yako kwa sababu inaharibu ngozi zaidi kwa kuinyima muonekano wake halisi,na inashauliwa kwa wale wasiopenda ama wasiojua kusoma lugha sahihi iliyoandikwa kwenye bidhaa husika ni vizuri kumuhusisha muuzaji kabla yakununua bidhaa hiyo na Kama imeandikwa kwa lugha ambayo haieleweki kwako na kwa muuzaji wa bidhaa tafadhali usinunue bidhaa hiyo. Pia tupende na kujenga mazoea ya kununua bidhaa hizi kwenye maduka maalum ili kupata bidhaa zenye ubora(original), ushauri zaidi na kusaidiwa endapo italeta matatizo.Ni vizuri na salama zaidi kutumia mafuta halisi yani yatokanayo na vitu halisi,Kama mafuta ya nazi(coconut oil),mafuta ya alovera (aloe oil) na mafuta ya mlonge(mlonge oil)bidhaa hizi hulimwa na kutengenezwa hapahapa nyumbani Tanzania na ni bidhaa bora sana kwa ngozi ya kila aina, huipa ngozi muonekano ang'aavu,laini na pia kukufanya uwe na ngozi bora ya kuvutia, rangi moja na mwenye afya zaidi.kumbuka kumuona na kumuhusisha daktari (doctor) endapo bidhaa hiyo itakusababishia madhara makubwa au magonjwa.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.