GAUNI NDEFU

Gauni ndefu humpendeza kila mtu (mwanamke) wa umbile lolote na urefu au kimo chochote, gauni hizi humfanya mwanamke avutie zaidi na kuwa na mwonekano wa kipekee na kwa upande mwingine humpa heshima zaidi. Nguo hizi huvaliwa mahali popote na muda wowote ilimradi tu iendane na mahali husika na muda muafaka, sio kila gauni refu linapendeza au linaweza valiwa usiku au kwenye sherehe na ndivyo hivyo sio kila gauni refu linaweza valiwa mchana au sehemu ya watu wengi, tukumbuke kila nguo inategemea na mahali unapoelekea na jinsi ilivyotengenezwa zipo gauni ambazo zimetengenezwa maalum kwa kuvaliwa usiku,zipo ambazo zimetengenezwa maalum kwa kuvaa mchana na nyingine kwenye shelehe na zingine zikiendana popote pale mtu anataka kwenda azibagui.Gauni ndefu zinapendeza kwa kitambaa chochote kile na rangi yoyote mtu mwenyewe atakayo pendelea na vile vile zipo zilizotengenezwa kwa kitenge na kuwa na muonekano wakuvutia(staili hii upendelewa zaidi na waafrika).katika urefu wa gauni inategemea mtu anapendeleaje kuna wengine hupenda urefu wa kawaida na ziwashikilie mwili na wengine hupendelea ziwe za mbuluzo na zisiwabane Sana.kwa muonekano wa gauni ni maamuzi ya mtu binafsi atakavyo pendezwa.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.