SHATI/BLAUZI FUPI (CROP TOPS)

BLauzi na shati fupi zimeenea Sana Kati Kati ya mwaka 2015 na ndio nguo zinazosadikika kuvaliwa Sana mwaka huu wa 2016,nguo hizi zimeonekana kupendwa Sana na kuvaliwa sana na wasichana wenye umri kuanzia miaka 30 kushuka chini yani ni vijana zaidi.Nguo hizi humfanya mwanamke aonekane nadhifu,mzuri na mwenye umbo la kuvutia zaidi kwa kuacha wazi sehemu ya tumbo mpka kiunoni, shati fupi zinauwezo wa kuvaliwa na nguo ya aina yoyote chini yaweza kuwa pensi,suruali,sketi na hata wengine wakizivalia juu ya magauni yenye uwazi Sana ili wawe huru zaidi. Nguo hizi zipo za aina tofauti kuna za jinsi (jeans),kitambaa,kitengee na hata za mpira,lakini tukumbuke kwamba nguo hizi zaweza tengenezwa kwa staili tofauti tofauti kimuonekano yaweza kua na mikono mirefu,mifupi au staili yoyote mtu aipendayo hukaa vizuri na kuvutia. Lakini pia nguo hizi huwapendeza zaidi wadada wenye matumbo madogo au wale wenye maumbile madogo kuanzia kwenye tumbo kushuka chini na pia wanene nao hazijawaacha mbali inategemea na mpangilio wa uvaaji wa mtu mwenyewe lakini pia tukumbuke nguo hizi zina mahala pake haswa kwa sisi watanzania sio kila sehemu waweza ivaa na ila pia inategemea unavaa vipi na kwa wale waendao ofisini au sehemu za maana zaidi waweza vaa kwa kuzingatia maadili pia kumbuka kuvaa nguo inayokufanya uwe huru.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.