VIPINI VYA PUA

Miaka ya nyuma ilizoeleka wanawake pekee ndo wanastaili kuvaa vipini puani na hata wengine kutoboa kabisa pua na kuweka vipini na wengi wao walipendelea zaidi kuvaa upande mmoja wa pua na mwingine kubakia kawaida. Lakini siku hizi imekua tofauti kidogo haswa hapa Tanzania na wanaume pia au jinsia yakiume wameanza kutumia urembo huu wa vipini puani na imeonekana kuwapendeza vile vile.Urembo huu umeanza muda kidogo na ulivaliwa sana na wanawake wa pwani na mara nyingi tulizoea kuwaona wa dini ya kislaam haswa wakipendeza na mtindo huu wa vipini,siku hizi imekua tofauti kidogo haswa tangu mwaka jana stahili hii imerudi kwa kasi zaidi na ubora wa hali ya juu. Sio watu wa pwani tu wanaotumia urembo huu hata wengine pia vile vile sio lazima kutoboa pua na kuvaa upande mmoja wa pua. Staili imekuja kivingine zaidi waweza vaa katikati ya pua Kama picha zinavyoonyesha haswa wanawake au kutoboa kabisa pua yakoy na kuweka kipini sehemu zote mbili za pua lakini wengi hupendelea Moja na kwa upande wa wanaume nimuhimu kutoboa kabisa ili kuweka muonekano mzuri na wakuvutia na waweza fanya hivyo kwa pande zote mbili za pua au upande mmoja tu na kufanya muonekano wa tofauti zaidi. Tukumbuke ni asilimia ndogo sana ya watu wanaokubaliana na muonekano huu Afrika haswa hapa nchini kwetu Tanzania na vile vile inakua ngumu zaidi kwa upande wa jinsia yakiume, tuwe makini katika hili japo urembo huu ni Kama urembo mwingine na umeanza tangu enzi za mababu zetu.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.