REMBA ZA KITENGE

Staili hii ni ya muda kidogo ila imekuja kivingine. Halo nyuma tulizoea kuona mtu akivaa nguo ya kitenge ndo anaweza weka remba au kitambaa kichwani cha kitenge kunakshi muonekano wake na staili hii ya kuvaa nguo za kitenge pamoja na remba lake tulizoea kuona kwa wa mama ndio wakipendelea staili hii lakini sio wa mama tu bali ni wa mama wakiafrika ndo walipendelea mavazi haya,lakini sasa imekua tofauti kidogo staili hii au mwonekano huu umekuja kivinge kabisa,waweza valiwa na nguo yoyote ile bila kujali ni yakitenge, kanga au laa cha muhimu kinatakiwa kuendana na muonekano wako na sehemu unayoelekea kwa muda huo. Lakini sio lazima kufunika nywele zote kichwani au kufunga kitenge kikubwa Sana waweza weka kidogo tu na kutengeneza muonekano wa tofauti kulingana na unavyopendelea mwenyewe.Staili hii sasa inapendelewa Sana na wasichana tofauti na hapo zamani lakini pia sio waafrika peke yake ndo wanaenda na muonekano huu lakini watu wa mataifa ya ulaya pia hatujawaacha nyuma nao wanavaa staili hizi nakuonekana nadhifu na kiafrika zaidi. Tukumbuke kwamba remba au kitenge kichwani kinavaliwa sehemu yoyote ile msibani,harusini, mtaani,ofisini, kwenye tamasha na kuendelea ni vazi ambalo halibagui na kuna baadhi ya watu huweka muonekano huu hata waendapo sehemu za ufukwe (beach)na huwapendeza zaidi ni jinsi wewe binafsi utapenda muonekano gani na kwa wale ambao hawawezi jifunga vitambaa kichwani waweza enda saluni kupata msaada zaidi au hata channel za YouTube huonyesha jinsi yakujifunga kiremba aina ya kitenge kichwani. Na kwa sisi waafrika muonekano huu unatupa heshima zaidi katika jamii zetu na kutufanya tuonekane wastaarabu zaidi haswa hapa kwetu Tanzania.Pia remba waweza valia na urembo tofauti tofauti haibagui ni wewe binafisi utakavyopendelea waweza ongeza urembo mwingine kichwani na hata hereni, cheni, bangili,saa na Pete sio lazima viwe vya kitamaduni zaidi waweza vyaa vya kawaida,na hata watoto wadogo jinsia ya kike nao waweza vaa remba au kitenge kichwani na kupendeza ptu,vitenge sio lazima kivaliwe na nguo yakitenge au kiwe cha kufanana waweza vaa tofauti na nguo ya kitenge uliyovaa ni jinsi yakuchanganya rangi tu.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.