MASHATI YA JINSI (JEANS)

Mashati ya jinsi yamependwa na kuvaliwa na jinsia zote wanawake kwa wanaumepia na watu wa umri tofauti tofauti wakubwa, vijana na watoto, nguo hizi zimewavutia wengi kutokana na kuwa kwenye muonekano na staili mbalimbali lakini pia mashati hya yapo kwenye ugawanyiko wa aina tofauti kuna mepesi ambayo uvaliwa mahali na muda wa joto lakini pia kuna ambayo ni mazito watu hupendelea kuvaa sehemu na muda wa baridi zaidi.vile vile mashati haya yapo kwenye muonekano mbali mbali kuna ya mikono mirefu, mikono mifupi na hata kata mikono, lakini pia nguo hizi zinaweza valiwa ofisini na kwenye sherehe mbali mbali inategemea na mtu mwenyewe anapenda Muonekano upi kwa muda huo. Shati hizi zaweza valiwa na kitu chochote chini na pia waweza ongeza vitu vya ziada kma vile mkufu,saa na bangili,ili kuleta muonekano tofauti nawakuvutia machoni kwa watu. Nguo hizi zinamwonekano na rangi nzuri tofauti na kuna nyingine zenye muonekano wa mpauko inategemea mtu anapenda ipi na sehemu anayoelekea atakopoivaa nguo hiyo ni maamuzi ya muhusika mwenyewe na anachopendelea kwa muda huo.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.