UREMBO/MWONEKANO WA NYWELE KWA WATOTO

Muonekano wa nywele ni kitu muhimu Sana na ndo kina mfanya mtu apendeze na kuonekana nadhifu, kila mzazi ana maono yake kuhusiana na mwonekano wa nywele za mtoto wake awe wa kiume au wa kike. Kuna vitu vingi vyakufanya mwanao au mtoto awe na muonekano nadhifu bila kutumia madawa ya kisasa ambavyo watu na wazazi wengi wanakimbilia.Dawa hizo sio sahihi kwa mtoto haswa wenye umri chini ya miaka minane japo kunabidhaa zinazokizi kwa matumizi ya mtoto kuanzia umri huo wa miaka minane na kuendelea.Mtoto hupendeza kwa staili mbalimbali waweza msuka nywele zake lakini kwa umakini na ufundi zaidi kwa sababu kichwa cha mtoto hakijakomaa Kama cha mtu mzima na kutokuwa makini kwaweza msababishia mtoto matatizo makubwa, pia waweza mchana nywele na kumuweka riboni (banio za nywele za mtoto) na kwa wakiume kumnyoa kimtindo zaidi ya kisasa lakini pia kutumia saluni maalum za watoto ambayo wanafanya kiuangalifu zaidi.staili zote hizo zitamfanya mtoto kuwa na muonekano wakuvutia lakini pia inashauliwa kutumia bidhaa asilia(mafuta ya nazi) na ambazo nimaalum kwa mtoto haswa kwa upande wa mafuta ya nywele ili kumfanya apendeze zaidi uku ukilinda afya ya mtoto.

No comments:

Post a Comment

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.