JINSI YAKUBANA NYWELE HALISI, KUTENGENEZA MAWIMBI (NATURAL HAIR)

Kubana nywele kuna kazi haswa kwa wale wenye nywele nyingi, nitaeleza hatua kwa hatua jinsi ya kuzifanya ziwe na mwonekano mzuri na kubana kwa urahisi zaidi. kwanza, zichane nywele zote vizuri mpaka zilainike.Mbili,zigawe mara tatu yaani Kama unabana mabutu (funga na vibanio).Tatu,chukua fundo moja peleka nyuma au hata Kati inategemea na staili unayobana(nyuma,Kati au pembeni).Nne malizia na lile fungu la mwisho kisha zifunge kwa kibanio maalum cha nywele, waweza zungusha mkia au ukaacha hivyo hivyo inategemea utakavyopendelea mwenyewe.kwa wale ambao wangependa kutengeneza mawimbi hatua ya kwanza,chana nywele zako vizuri mpaka zinyooke na uzipake mafuta maalum kwa ajili ya nywele (ya maji au mgando). Pili,kata nywele katika mafungu madogo madogo na kuzisuka mabutu(njia tatu au mbili) ni muhimu kuweka rola kama ukizilowanisha kwa maji kidogoKama unavyoona pichani au usiweke.Tatu,kaa nazo kuanzia SAA moja na kuendelea(ili zikauke vizuri kwa waliotumia rola na maji kidogo) na kwa wale ambao hawata tumia rola waweza lala nazo kama huna mahali pa kwenda kwa muda huo au Kama umefanya usiku.Nne,toa rola(Kama uliweka) na chambua vizuri kwa mkono au chanuo yenye nafasi kubwa ili usiharibu mawimbi ya nywele.

           
SOMA

RASTA ZA NJIA TATU AU MBILI (BRAIDS)

Nywele hizi husukwa kwa kutumia rasta, kwa urefu wowote mtu atakaopenda lakini pia na rangi utakayo chagua mwenyewe.Hutengeneza muonekano mzuri na unaweza kwenda nazo mahali popote pale ni jinsi tu utakavyo zibana,jambo muhimu la kuzingatia unaposuka rasta hizi kwanza, hakikisha msusi wako asizishike nywele za mbele kabisa(malikia) wakati wa kusuka zitasababisha kukatika kwa nywele za mbele lakini pia maumivu makali. Pili,akikisha unapakwa au unapaka mafuta nywele zako lakini pia rasta zenyewe uzipake mafuta ili kupunguza ukavu ambao unaweza sababisha kukatika kwa nywele zako.Tatu na mwisho hakikisha haukai na nywele hizo zaidi ya wiki tatu zinaweza pelekea kukatika kwa nywele na kusababisha harufu mbaya kichwani.Furahia nywele zako kwa kubana staili yoyote Kama picha zinavyojieleza.
SOMA

AINA ZA NGONZI NA MATUNZO YAKE

Kuna aina nne za ngozi (muonekano) kwa jinsia zote mbili yani kike na kiume.Aina zote hizi zinaitaji matunzo tofauti tofauti kulingana na mtu mwenyewe, unaweza fanya mwenyewe au Kama una uwezo zaidi kwenda kufanyiwa sehemu maalum Kama saloon.Tukumbuke pia kwenye matumizi ya vitu Kama mafuta na losheni( lotion) za mwili ni muhimu kuzingatia una ngozi ya aina gani na hata bidhaa zenyewe huwa zimeelezwa matumizi sahihi yaani inastahili ngozi ya aina gani, kwa hilo ni muhimu zaidi kuzingatia ili kupata muonekano sahihi unaoitaji.Aina ya kwanza Kama inavyoonekana pichani ni ngozi kavu(Dry skin),yaani isiyo na mafuta, watu wenye aina hii ya ngozi hupata shida sana kwa sababu ngozi inapokua kavu husababisha kuvutana,mipasuko,ugumu na kusinyaa!watu wenye aina hii ya ngozi hushauliwa kupaka lotion au mafuta ya kulainisha ngozi(for dry skins) ili kuwafanya wawe na muonekano ng'aavu na wakuvutia. Aina ya pili ni ngozi ya kawaida(Normal skin),aina hii ya ngozi inakua na mafuta kidogo na ukavu kidogo ni wachache sana wenye aina hii wanaojigundua kua nyuso zao zinamuonekano mara mbili.mtu yeyote mwenye aina hii ya ngozi anashauliwa kupaka mafuta yakawaida yasiokua makavu sana na wala yenye mafuta sana Kama nilivyoeleza hapo mwanzo mafuta ama losheni( lotion) mara nyingi hua zimeandikwa kama itakuwia vigumu sana kusoma ni vizuri kumuuliza muuzaji wa bidhaa hiyo. Aina ya tatu ni ngozi ambayo katikati hua inamafuta yaani paji la uso kushuka mapaka kwenye pua na pembeni kuwa na ngozi ya kawaida(Combination skin),aina hii ya ngozi inaitaji umakini sana kwa sababu unaweza dhani ngozi yako ni ya mafuta kumbe sio yote ni vizuri na ni salama kuhusisha wataalam wa urembo kwenye uchaguzi wa mafuta au losheni(lotion) epuka sana kupaka vitu vyenye mafuta na vikavu pia,yaani iwe ya kawaida. Aina ya nne ni ngozi yenye mafuta(Oil skin),aina hii ya ngozi haiitaji kabisa kupakwa mafuta ama losheni zitakazo ongeza mafuta zaidi  kwenye ngozi kwa sababu itazidisha zaidi na ni vizuli kutumia losheni(lotion)kavu ili kupunguza mafuta hayo na kuipa ngozi muonekano sahihi.Hakikisha unatumia bidhaa sahihi kwa aina yako ya ngozi na epuka kutumia bidhaa zitakazo badili(chubua) ngozi yako kwa sababu inaharibu ngozi zaidi kwa kuinyima muonekano wake halisi,na inashauliwa kwa wale wasiopenda ama wasiojua kusoma lugha sahihi iliyoandikwa kwenye bidhaa husika ni vizuri kumuhusisha muuzaji kabla yakununua bidhaa hiyo na Kama imeandikwa kwa lugha ambayo haieleweki kwako na kwa muuzaji wa bidhaa tafadhali usinunue bidhaa hiyo. Pia tupende na kujenga mazoea ya kununua bidhaa hizi kwenye maduka maalum ili kupata bidhaa zenye ubora(original), ushauri zaidi na kusaidiwa endapo italeta matatizo.Ni vizuri na salama zaidi kutumia mafuta halisi yani yatokanayo na vitu halisi,Kama mafuta ya nazi(coconut oil),mafuta ya alovera (aloe oil) na mafuta ya mlonge(mlonge oil)bidhaa hizi hulimwa na kutengenezwa hapahapa nyumbani Tanzania na ni bidhaa bora sana kwa ngozi ya kila aina, huipa ngozi muonekano ang'aavu,laini na pia kukufanya uwe na ngozi bora ya kuvutia, rangi moja na mwenye afya zaidi.kumbuka kumuona na kumuhusisha daktari (doctor) endapo bidhaa hiyo itakusababishia madhara makubwa au magonjwa.
SOMA

JINSI YAKUJIFUNGA KIREMBA CHA MDUARA NA HIJABU KWA NJIA YA PICHA


SOMA

BUCKET BAGS/MIKOBA AINA YA NDOO

Mansur Gabriel's ndo mbunifu wa mikoba aina hii,mikoba hii imekaa Kama ndoo yani muonekano wake Kama ndoo na ipo tofauti kabisa na aina nyingine nyingi za mikoba tuliyoizoea. Mikoba hii ipo ya aina tofauti na ukubwa tofauti nikimaanisha kuna ya ngozi na vitambaa na pia kuna mikubwa na midogo,kwa hapa Tanzania mikoba hii haijabebwa Sana haswa na watu maarufu kuifanya ijulikane zaidi lakini tegemeo la wabunifu wengi,wanamitindo na wafatiliaji na wapenda mitindo tunategemea kuiona mwaka huu 2016 mpaka mwaka 2017 kwa watu wa aina tofauti ikilengwa zaidi kwa wanawake.Mikoba hii inauwezo wakubeba vitu vingi zaidi na no imara kwa jinsi ilivyotengenezwa na kuvalia kwa nguo yoyote ile na mahali popote pale ila kwa kuzingatia rangi mahali unapoenda na ukubwa wa mkoba wenyewe
SOMA

NYWELE ZA AFRO

Afro ni nywele maarufu zenye muonekano wa kiafrika zaidi, nikimaanisha kuwa waafrika ndo wenye nywele za aina hizi tofauti na watu wa bara la ulaya yani wazungu,nywele hizi hua zinamwonekano wa kujaa zaidi zipo ndefu na fupi pia yani zenye urefu wa kawaida tu,vile vile nywele hizi zipo za kushonea kwa wale ambao hawana aina hii ya nywele lakini pia kuna baadhi ya watu wananywele hizi halisia kabisa yani zisizo za kushonea wala kuvaa. Mara nyingi nywele hizi huwa hazitakiwi kuchanwa haswa zile zisizo halisia yani zakushonea au kuvaa,hupakwa mafuta ya nywele na kuvutwa tu kwa mkono na kukaa sawa lakini kwa wale ambao nizahalisia huchanwa Kama kawaida na haziwezi badilika wala kuharibika kwa sababu ndo uhalisia wake huo.nywele za afro humpendeza kila mtu na hutengenezwa na kubanwa kwa staili mbalimbali inategemea na mtu mwenyewe hupendelea muonekano upi wa nywele zake kwa muda huo, na kwa wale wakutengeneza ambazo sio halisi nywele hizo zipo za rangi tofauti tofauti inategemea na mtu mwenyewe hupendelea vipi. Nywele za aina hii hutumiwa pia na wanaume(kwa nadra Sana) mara nyingi Kama kuna kitu muhimu Kama kurekodi vipindi maalum vya kuchekesha na hata filamu.
SOMA

NGUO ZA KUOGELEA KWA KINA DADA (SWIMING COSTUMES)

Hizi ni nguo maalum zakuogelea na kuendea sehemu za ufukwe nguo hizi mara nyingi huacha sehemu kubwa ya maumbile ya mwanamke wazi ila humfanya awe huru zaidi katika zoezi hilo vilevile hizi ni nguo ambazo maalum zimetengenezwa kwa ajili ya zoezi hilo. Nguo hizi zipo za aina tofauti tofauti zipo chupi na blazia zake na zipo za moja kwa moja kuanzia juu mpka chini yani iliyoungana.inategemea muhusika mwenyewe atapenda nguo zipi Kati ya hizo mbili, lakini pia imekua tofauti kidogo nguo hizo waweza valia suruali au kitu kingine kwa chini haswa zile za moja kwa moja na kuna baadhi ya watu hutumia kufanyia mazoezi haswa wale wanaopendelea kufanya mazoezi ufukweni inakua ikiwapa uhuru zaidi(kama picha zinavyoonyesha)na kwa chupi na blazia kuna baadhi ya watu hutumia Kama nguo za ndani kawaida japo hutegemea zaidi na muundo wa nguo yenyewe na kuna wengine hutumia nguo za ndani walizonazo zinazoendana vizuri nacho sio kitu kibaya. Nguo hizi zinaumuhimu kwa mwanamke kuwa nazo katika kabati lake na tukumbuke kuwa kuogelea hufanya ngozi kuwa nyororo na laini pia hupunguza vipele na harara mwilini na nizoezi tosha kwa watu wasiopenda kufanya mazoezi mengine, ngozi ikiwa laini pia huwezesha vitu vingine Kama mafuta ya mwili kufanya kazi kwa ufasaha na kuleta matokeo mazuri ya ngozi yako. Ikumbukwe kuwa sio kila mtu anaetaka kwenda ufukweni ni lazima kuvaa nguo hizo ni kwa wale wanaoweza tu na haswa kwa sisi watanzania inakua ngumu kidogo kutokana na maadili ya baadhi ya familia zetu japo sio kitu kibaya kufanya cha muhimu kiendane na mazingira halisi ya tendo lenyewe.

SOMA

Content Copyright © 2016 by Flaviana Maguha All rights reserved.